LST Yashiriki Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani
LST Yashiriki Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani
13 Mar, 2024
Watumishi wanawake wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School) wameungana na wanawake wenzao kote ulimwenguni kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ambayo hufanyika tarehe 8 Machi kila mwaka.
Katika kusherehekea siku hiyo maalum, wanawake hao pia walipata fursa ya kutoa msaada wa kijamii kwa kupeleka baadhi ya mahitaji muhimu kwa wagonjwa katika Hospitali ya Sinza jijini Dar es Salaam.
Sambamba na hayo, wanawake wa LST pia wameshiriki katika sherehe za kuadhimisha siku hiyo zilizofanyika kimkoa wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Kaulimbiu ya Siku ya Wanawake mwaka huu ni "Wekeza kwa Wanawake Kuharakisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii".