Ujumbe kutoka Kamisheni ya Umoja wa Afrika (Africa Union Commission) ulitembelea Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (LST) tarehe 22 Mei, 2026 jijini Dar es Salaam.
Ujumbe huo uliongozwa na Mshauri wa Sheria na Kaimu Mkurugenzi wa Itifaki wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Prof. Hajer Gueldich ambaye aliongozana na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Dunia ya Haki, Mhe. Abdulqawi A. Yusuf, Afisa Mkuu wa Sheria wa Umoja huo Bi. Mtendere Gondwe pamoja na Afisa Sheria Mshiriki wa Umoja huo, Bw. Stephen Buabeng-Baidoo.
Ujumbe huo uliongea na Menejimenti kuhusu dhumuni la ziara yake na majukumu yanayotekelezwa na Taasisi. Pia ujumbe huo ulipata fursa ya kuongea na wanafunzi wa kundi la 42 kuhusu mfumo wa utoaji haki wa Umoja wa Afrika.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) Mhe. Hamza Johari (katikati) akishuhudia makabidhiano ya hati ya makubaliano ya kuimarisha mashirikiano baina ya Ofisi yake na Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (LST). Hafla hiyo imefanyika tarehe 2 Julai, 2025 jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Samwel Maneno na kulia ni Mkuu wa Taasisi ya LST Prof. Sist Mramba.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania - Divisheni ya Kazi, Mhe. Jaji Dkt. Yose Mlyambina amekabidhi juzuu za maamuzi ya migogoro ya kazi kwa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (LST). Juzuu hizo zimepokelewa na Mkuu wa Taasisi ya LST, Prof. Sist Mramba na zinatarajiwa kuwasaidia wanafunzi, watafiti na wadau mbalimbali wa masuala ya sheria kupata rejea sahihi na tafsiri za kisheria katika migogoro ya kazi. Makabidhiano hayo yamefanyika tarehe 10 Oktoba, 2025 katika Ofisi za LST jijini Dar es Salaam ambapo yalishuhudiwa na baadhi ya Watumishi wa Mahakama Kuu pamoja na LST.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Juma Homera (aliyesimama katikati mstari wa mbele) akiwa na Menejimenti pamoja na Watumishi wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (LST) alipotembelea LST kwa ziara ya kikazi tarehe 12 Desemba, 2025. Katika ziara hiyo aliambatana na Naibu Waziri Mhe. Zainab Katimba pamoja na Naibu Katibu Mkuu Dkt. Franklin Rwezimula.
Wanafunzi wa Law School wakiwa kwenye mafunzo kwa vitendo
Baadhi ya wahitimu wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (LST) wakila kiapo cha Uwakili mbele ya Jaji Mkuu wa Tanzania.